MVULANA WA MIAKA 10 AOKOLEWA SAA 8 BAADA YA KUKWAMA KWENYE GARI LA TAKATAKA


Umati wa watu ulikusanyika wakati waokoaji walipokuwa wakijaribu kumuoka mvulana usiku

***
Mvulana mwenye umri wa miaka 10-ameokolewa saa nane baada ya kukwama katika lori la takataka katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.

Mvulana huyo aliyetambuliwa na polisi kama Majed Mubarak Ibrahim, alikuwa akifaya kazi na lori linaloendeshwa na kampuni ya usafi ya taifa - Khartoum State Cleaning Corporation.

Inaaminiwa kuwa alivutwa ndani ya lori alipokuwa akitupa takataka.

Kwa sasa yuko hospitalini, lakini polisi haijatoa maelezo zaidi kuhusu hali yake.

Watu walishirikishana picha kwenye mitandao ya kijamii za wahudumu wa uokoaji wakiendelea usiku mzima kujaribu kumuokoa mvulana huyo.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema viganja vya mtoto vilikuwa vinaonekana-huku akiwa amekwama katika vifusi vya vyuma vikuu kuu.

Moja ya picha fupi ya video ya tukio hilo ilionyesha mtu mmoja akijaribu kupasua chuma, huku mwingine akihjaribu kulazimisha kufungua lori.

Umati wa watazamaji waliokuwa wakishuhudia tukio hilo ulizingira gari-huku wengine wakitoa ushauri kuhusu namna ya kumuokoa mtoto.

Jumbe za mitandao ya kijamii zinasema ajali hiyo inatoa mwangaza wa tatizo la ajira kwa Watoto nchini sudan, ambako mara kwa mara Watoto hutumiwa vibaya na baadhi huajiriwa kama wanajeshi.

Hali ngumu ya kiuchumi nchini Sudan imewafanya baadhi ya Watoto kufanya kazi hatari.

Kuna idadi kubwa ya watoto wa mitaani katika mji mkuu Khartoum na miji mingine mikubwa.

Kulingana na Shirika la Watoto la Umoja wa mataifa (Unicef), Watoto wa Sudan wapatao milioni tatu hawaendi shule.

Wanafanya kazi mbali mbali kama vile, usafi, kuuza bidhaa mitaani, kutengeneza matofali na kukusanya takataka - wakiwa katika hatari ya kutumikishwa vibaya na kunyanyaswa.

Malipo duni na hali mbaya ya kazi katika shirika la usafi la - Khartoum State Cleaning Corporation pia imeelezewa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya Habari ya kijamii, huku wafanyakazi walioajiriwa na kampuni hiyo wakiandamana hivi karibuni.

Mmoja wa wanaharakati, El-Sadiq Eissa,alituma ujumbe wa Twitter kuhusu jinsi alivyokutana na mfanyakazi wa zamani wa kampuni ambaye mguu wake ulikatwa kufuatia ajali aliyopata kazini.


Kulingana na mwanaharakati huyo, mwanaume huyo sasa ni omba omba kwenye mitaa ya Khartoum baada ya kamouni kukataa kulipia garama za matibabu yake.

Chanzo- BBC Swahili


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments