YANGA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Sunday, January 16, 2022

YANGA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI, YAICHAPA COASTAL UNION 2-0


***************


EMMANUEL MBATILOKlabu ya Yanga Sc imefanikiwa kuondoka na alama tatu mara baada ya kufanikiwa kuichapa Coastal Union ya Tanga kwa mabao 2-0 katika dimba la Mkwakwani Tanga.

Yanga Sc ilianza kupata bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa DR Congo Fiston Mayele ambaye alimalizia krosi iliyopigwa na beki Djuma Shabani dakika ya 40 ya mchezo.

Goli la pili la Yanga liliwekwa kimyani na Said Ntibazokiza dakika ya 90 ya mchezo akipokea pasi murua kutoka kwa Farid Mussa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages