SIMBA WAAMBUKIZWA CORONA


KATIKA hali isiyo ya kawaida, Simba na Puma katika mbuga ya wanyamapori nchini Afrika Kusini imeelezwa kuwa huenda wameambukizwa virusi vya corona ambavyo vinaitesa dunia kwa sasa.

Taarifa hiyo imetolewa na wamiliki wa wanyama hao baada ya utafiti uliofanywa na wanasayansi katika chuo Kikuu cha Pretoria.

Wanasayansi hao wameonya kuhusu hatari ya kirusi kipya kutokea iwapo virusi hivyo vitasambaa katika hifadhi nyingine za Wanyama na kusambazwa tena kwa binadamu.

Utafiti huo ulifanywa baada ya Wanyama hao kuugua na dalili ambazo zinafanana na zile za virusi vya corona kwa binadamu ikiwemo tatizo la kupumua , kutokwa na kamasi na kikohozi kikavu.


Vipimo vilivyofanyiwa Wanyama hao vilionesha kwamba wameambukizwa corona, watafiti hao walisema, wakati ripoti zikisema kwamba waliambukizwa ugonjwa huo na wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia.

Watafiti hao waliongezea kwamba wahudumu wa hifadhi hizo za Wanyama walikuwa na virusi vya corona walivyosambaziana wakati huo lakini hawakuonesha dalili zozote.



Wamependekeza hatua kama vile kuvalia barakoa wakati wanapowahudumia Wanyama hao. Utafiti huo umechapishwa katika jarida la virusi la Peer Review.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments