WALIOMUUA BALOZI WA ITALIA NCHINI DRC WAKAMATWA

Jeshi la Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Jimbo la Kivu Kaskazini, limefanikiwa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa wanaodaiwa kushiriki katika mauaji ya aliyekuwa balozi wa Italia nchini humo, Luca Attanasio.

Wakiwakabidhi mbele ya gavana wa kijeshi wa Jimbo la Kivu Kaskazini, maafisa wa polisi wamewataja watuhumiwa hao kuwa ni Bahati Kiboko na Balume Baluku huku juhudi za kuwasaka watuhumiwa wengine, akiwemo kiongozi wao anayefahamika kwa jina bandia la Mr Aspirant, zikiendelea.

Polisi wamesema watuhumiwa hao na wenzao, waliuteka msafara wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) katika eneo lijulikanalo kama 3 Antennas katika Barabara ya Goma- Rutshuru, katika Hifadhi ya Virunga Februari, 2021 na kuwateka watu kadhaa akiwemo balozi huyo.

Polisi wameendelea kueleza kuwa lengo la watuhumiwa hao, lilikuwa ni kulipwa fidia lakini iliposhindikana, ndipo walipompiga risasi balozi huyo na kusababisha kifo chake saa kadhaa baadaye.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post