MWALIMU MSTAAFU AFARIKI BAADA YA KUJIBURUDISHA NA MREMBO GESTI

Polisi kaunti ya Nakuru nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo mwalimu aliyekuwa amestaafu aliaga dunia kwa njia ya kutatanisha baada ya kujiburudisha na mwanamke katika lojing'i (Gesti).

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76 alikuwa amelipia chumba cha kulala katika hoteli ya Salama logde usiku wa Jumatano, Januari 5,2022 na baadaye akajiunga na mrembo mmoja majira ya saa sita usiku. 

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ambao walifika katika la kisa Alhamisi asubuhi, waliarifiwa kwamba mwanaume huyo alikuwa amekunywa pombe ya kienyeji kupita kiasi.

 Mhudumu mmoja ambaye alikuwa akiendelea na majukumu yake aliungudua mwili wa mzee huyo kitandani baada ya kupata mlango wa chumba hicho ukiwa umefungwa kwa ndani.

"Mara moja alimfahamisha meneja Bernard Kiarie, ambaye aliwajulisha wapelelezi wetu walioko Molo, kuhusu tukio hilo," wapelelezi walisema.

 Katika kisa kingine sawia na hicho mwanaume mmoja aliyetambuliwa kama Clinton Wanakacha mwenye umri wa miaka 26 alipatikana amefariki dunia katika chumba cha sita cha nyumba ya wageni ya Miathathia asubuhi ya Jumanne, Januari 4, 2022.

 Mfanyakazi wa chumba hicho aliwaambia wapelelezi kuwa marehemu aliingia chumbani humo usiku uliopita mwendo wa saa nane mchana. 

Alikuwa ameandamana na mwanamke ambaye bado hajatambulika. Baada ya makachero kufanya uchunguzi wao katika eneo la tukio walipata mipira miwili ya kondomu ikiwa chini ya kitanda. 

Mwili wa Wachanaka ulipelekwa katika makafani ya City kusubiri upasuaji.

Chanzo - Tuko News blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments