MTALII AKANYANGWA NA TEMBO HADI KUFA


MTALII mmoja amekanyagwa hadi kuuawa na Tembo katika mbuga ya wanyama nchini Uganda, baada ya mtalii huyo kutoka kwenye gari alilokuwa akisafiria tukio hilo lilitokea Jumanne usiku.

Marehemu, ambaye ni raia wa Saudia, alikuwa akitalii kwenye mbuga ya taifa ya wanyama ya Murchison Falls National Park iliyopo katika mji la Arua.

Inadaiwa kuwa marehemu pamoja na wenzake waliposimama kujisaidia. na alikwenda mbali zaidi ya gari, hakuweza kurejea.

Maafisa wa mbuga ya Wanyama walithibitisha tukio hilo na walisema upelelezi unaendelea walisema kuwa hatua zinachukuliwa kuzuwia matukio ya aina hiyo kutokea tena.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments