MRADI WA AKILI BANDIA WAZINDULIWA UDOMSerikali ya Tanzania imezindua mradi wa maabara ya akili bandia (artificial intelligence) utakaosaidia kurahisisha shughuli za maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu Januari 24, 2022 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah akizindua mradi huo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

“Kama hivi wengi tunavyoangalia dunia za sasa hivi wenzetu wameshakwenda mbele zaidi. Sometimes (wakati fulani) unakuta watu wanavyokwenda makazini wanajibiwa na robot, unapopanda lifti, mwendo kazi,” amesema.

Naibu Waziri huyo amesema teknolojia hiyo inatumika hata mashambani ambapo badala ya kwenda mtu linatumika robot na maofisini.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments