AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUIBA MBWA WA JAMAA YAKE




MWANAUME mmoja kutoka Kaunti ya Nairobi, aliyefahamika kwa jina la Ian Kinuthia ana hadi Februari 7, mwaka huu kujua hatima yake baada ya kushtakiwa kwa kumuiba mbwa wa jamaa yake.

Ian alifikishwa mbele ya Mahakama ya Kibera jana Jumanne, Januari 25, na baada ya kusomewa mashtaka hayo akituhumiwa kuvamia Boma la Elizabeth Wambui na kuhepa na mbwa wake na kwenda kumuuza kwa Ksh 100,000 (sawa na zaidi ya Tsh milioni 2).


Hakimu mkazi Renee Kitangwa alielezwa kwamba Wambui ambaye hakuwepo nyumbani, alirejea siku hiyo na kugundua mbwa wake hayupo ndani ya nyumba yake, alianzha msako na kupewa taarifa kuwa wanaume wawili walionekana wakitafuta soko mbwa lakini walitimuliwa.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mbele ya hamiku, Kinuthia alikana mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Ksh 100,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post