MAKADA 71 WA CCM WAJITOSA USPIKA KUMRITHI JOB NDUGAI...WANAUME NI 60 , WANAWAKE 11


Jumla ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 71 wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kujaza nafasi ya Aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu hivi karibuni.

 Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Januari 15,2022 Jijini Dodoma ikiwa ni siku ya mwisho ya uchukuaji fomu, Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomoni Itunda amesema kati ya makada hao 71 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu kati yao wanaume ni 60, wanawake wapo 11.


Itunda amesema kwa siku ya leo jumla ya wanachama watano walichukua fomu na kufanya idadi kufikia wanachama 71 baada ya wale 66, waliokuwa wamechukua hadi jana Ijumaa Januari 14,2022.

“Leo hii tumepokea wanachama watano ambao wamejitokeza katika vituo vyetu vya Dodoma na Dar es saalam kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hii ya Uspika iliyoachwa wazi",amesema.

Amesema katika kituo cha Dodoma mwanachama mmoja ndiye aliyejitokeza kuchukua fomu wakati katika ofisi ya Lumumba ni wanachama wanne na afisi kuu ya Zanzibari hakuna aliyechukua fomu.Amesema kukamilika kwa zoezi hilo la kuchukua fomu lililoanza Januari 10 mwaka huu kunatoa nafasi kwa vikao vingine kuanza.

“Baada ya zoezi hili la kuchua na kurejesha fomu sasa hatua inayofuata ni vikao vingine kuketi ili kuanza kufanya mchujo wa kupitisha jina moja litakalo kiwakilisha chama katika kugombania nafasi hii ya Uspika”,ameeleza.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments