MWANAMKE AJIFUNGUA BAADA YA MIAKA 20 YA KUWA TASAShangwe na vigelegele zimeshamiri nyumbani kwa mwanamke mmoja nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 51, baada ya kujifungua watoto kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20 katika ndoa.

Mwanamke huyo, Justina Bassey, alijaliwa watoto pacha wa kike na kiume baada ya kuwa tasa zaidi ya miaka 20.

Mama huyo aliyetambuliwa kwa jina Justina Bassey, alijaaliwa watoto pacha wa kike na wa kiume baada ya kuwa tasa zaidi ya miaka 20. Taarifa hizo zilifichuliwa na rafiki wa karibu wa mama huyo Felicia Odey, kupitia Facebook akisema,

“Kile ambacho Mungu hawezi kufanya hakika hakipo. Tafadhali familia ungana nami kusherehekea na dada huyu, rafiki na mfanyakazi mwenzangu ambaye Mungu alimkumbuka na kumbariki kwa mapacha baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka ishirini na umri wa miaka hamsini na moja. Familia yangu namshukuru Mungu na kusherehekea pamoja na familia yako. BI JUSTINA BASSEY. Hongera sana!!!”Katika simulizi nyingine ya kutafuta watoto, Familia moja yakosa usingizi kufuatia kutoweka kwa mtoto wao aliyekwenda kwa mganga kutafuta mtoto, ambapo ameshindwa kuoga kwa miaka 4.Katika kutafuta taarifa tofauti kuhusu uzazi, baada ya kujaribu miaka kadhaa kupata mtoto bila mafanikio, Fatuma alishindwa kustahimili presha ya wakwe zake na kumtembelea mganga ambaye alimchanja dawa fulani za kiasili mwilini.Mnamo mwaka wa 2000, azma ya moyo wa Fatuma ilitimizwa wakati alijaliwa mtoto lakini furaha yake ilikuwa ya muda mfupi baada ya kumpoteza malaika huyo.Ni katika harakati hii ndipo Fatuma alishindwa kustahimili presha ya wakwe zake na kuamua kutafuta huduma za mganga na hata hivyo, kile kilionekana kuwa matumaini kwa Fatuma kiligeuka kuwa jinamizi na kumfanya kuanza kupagawa na sasa anaishi na maumivu kila mara.Jambo ambalo linamsumbua Fatuma zaidi ni kwamba huwa anaugua kila mara na pasi ya kutokuwa na ajira, sasa hana uwezo wa kufanya kazi za kijungu jiko ambazo alikuwa akizifanya mbeleni kupata riziki.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments