MIILI YA WANAWAKE WATATU WALIOUAWA NA KUTUPWA JIJINI MWANZA YAZIKWA


Miili ya watu watatu wa familia moja waliouawa jijini Mwanza imezikwa mjini Sengerema leo Januari 21,2022.

Akiongoza ibada ya maziko nyumbani kwa marehemu Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Imakulata Bomani mjini humo, Padri Fred Mgabi amesema waliofanya mauaji hayo hawana hofu ya Mungu na hawajawahi kufika kanisani na kwamba hukumu yao wataikuta kwa Mungu kutoka na matendo yao.

Tukio la wanawake watatu kuuawa kikatili kisha miili yao kutupwa, lililotokea Januari 19, 2021 katika Mtaa wa Mecco Kusini, Kata ya Mecco jijini Mwanza.

Waliouawa ni Mary Charles, Janeth Fred pamoja na Monica Jonas na miili yao ilipowasili wananchi waliangua vilio kutokana na mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments