WAZIRI ATOA SIKU TATU UCHUNGUZI KUPANDA KWA BEI YA SODA NA VIFAA VYA UJENZIWaziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashantu Kijaji
***

Tume ya Ushindani nchini (FCC) imetakiwa kutoa sababu za kupanda kwa bei za vinywaji baridi ndani ya siku tatu.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ashantu Kijaji kufuatia hali ya kuadimika na kupanda kwa bei ya vinywaji baridi ikiwemo soda.

Wakati huohuo, waziri Kijaji ametoa muda wa siku 7 kwa Tume ya Ushindani kutoa sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na kueleza hatua zilizochukuliwa na tume hiyo kukabiliana na hali ya kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments