RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE AJALI ILIYOUA WATU 14, WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameeleza kushtushwa na ajali iliyosababisha vifo vya watu 14 mkoani Mwanza.

Mheshimiwa Rais Samia ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akimuomba Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka.

"Nimeshtushwa na vifo vya Watu 14 wakiwemo Wanahabari 6 vilivyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugonga na Daladala. Poleni Wafiwa, Wanahabari na jamaa wote. Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu na Majeruhi wapone haraka,"ameeleza Mheshimiwa Rais Samia.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili likiwemo la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara baada ya kugongana uso kwa uso leo Janauri 11, 2022.


Tayari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, ameahirisha ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments