YANGA YAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI NBC PREMIER LEAGUE, YAICHAPA BIASHARA UNITED 2-1***************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Yanga imeendelea kusalia kileleni mwa ligi kuu NBC mara baada ya kufanikiwa kuwachapa Biashara United kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Biashara United ilifanikiwa kupata bao la mapema mara baada ya kipa wa Yanga kupigiwa shuti kali na kutena na mchezaji wa Biashara United kumalizia.

Yanga ilianza kutawala mchezo kutafuta goli la kusawazisha hivyo baadae mshambuliaji raia wa DR Congo Fiston Mayele kupachika goli kali lililokwenda mpoja kwa nyavuni na kwenda mapumziko Dubai ukisomeka 1-1.

Kipindi cha pili mchezo ulibadilika kwa Biashara United kuchezea nafasi nyingi za mabao ambazo zingezaa mabao ya kutosha.

Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji wao ambapo alitoka Farid Mussa na nafasi yake ikachukuliwa na Jesus Muloko ambaye alikuwa mwiba kwa timu wapinzani kwani alisababisha kuzaa kwa penati ambayo Said Ntibazokiza alifunga na kuiwezesha timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 2-1.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments