TUMBILI WAFANYA KISASI, WAUA MBWA 250 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, December 24, 2021

TUMBILI WAFANYA KISASI, WAUA MBWA 250Hizi ni ripoti kutokea Maharashtra, nchini India, ambapo kundi la tumbili limelipiza kisasi kwa kuwaua mbwa wapatao 250, baada ya kukasirishwa na kitendo cha mbwa kumuua kichanga chao.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa, tumbili hao walitekeleza mauaji hayo kwa kuwakamata mbwa na kupandanao juu ya miti kwenye nyumba na kisha kuwatupa chini.

Tayari mamlaka za wanyama pori nchini humo zimefika eneo la tukio na kuwakamata tumbili hao na kuwaweka kwenye uangalizi maalumu.

Ushawahi kukutana na timbwili la tumbili?

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages