ASKARI ALIYEPANDISHWA CHEO KWA KUKATAA RUSHWA YA MILIONI 10 APEWA ONYOMeshack Samson anayefanya kazi Arusha alipandishwa Cheo kutoka Sajenti (Sgt) hadi Stesheni Sajenti (Ssgt) mwaka 2019 baada ya kukataa rushwa ya Tsh. Milioni 10.

Askari huyo ameshushwa cheo kutokana na kutotii Mamlaka ya kwenda Kozi ya Kipolisi kuendana na Cheo alichopewa, ikielezwa hakuwa na sababu za msingi kukataa kufanya hivyo.

Ameshushwa ngazi moja kutoka Stesheni Sajenti kuwa Sajenti wa Polisi baada ya kushtakiwa na kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kwa kukataa amri halali ya Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post