TBS YAWAPATIA MAFUNZO WADAU WA NYAYA ZA UMEME MKOA WA DAR ES SALAAM - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, December 21, 2021

TBS YAWAPATIA MAFUNZO WADAU WA NYAYA ZA UMEME MKOA WA DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam. Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Bw.Hamisi Mwanasala akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam. Kaimu Meneja Viwango TBS Bi.Nasra Yusuf akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika Mkoa wa Dar es Salaam.Wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na TBS kwaajili ya kuwajengea uwezo waweze kutengeneza, kuuza, na kusambaza nyaya za umeme zilizokidhi viwango

*********************

NA EMMANNUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa mafunzo kwa wadau wa nyaya za umeme wanaojishughulisha na utengenezaji, uagizaji, usambazaji uuzaji na watumiaji wa nyaya za umeme katika mkoa wa Dar es Salaam ili kuhakikisha wanatengeneza nyaya ambazo zinakidhi viwango na ubora unaotakiwa.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema amesema ikiwa mtumiaji hawezi kupata nyaya za umeme zenye ubora itasababisha kuwepo kwa malalamiko juu ya thamani ya maisha yao na fedha zao.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwashirikisha washiriki ili wawe kwenye muelekeo mzuri zaidi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika pamoja na huduma wanazotoa kwa jamii.

"Warsha hii imewalenga wadau wa makundi wasiopungua 30 kutoka mkoa wa Dar es Salaam na kwa hadhara hii napenda kusema kwamba tumetiwa moyo sana kwa mwitiko wa mwaliko wetu mliouonesha". Amesema

Aidha amesema wataendelea kushirikiana na wadau wa nyaya za umeme nchini ili kuhakikisha wanaweza kuzalisha nyaya zenye ubora unaotakiwa kwa watumiaji wa nyaya za umeme.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages