Breaking

Post Top Ad

Friday, December 31, 2021

MWANAMKE AJIFANYA KAHABA, AWALEWESHA WANAUME KISHA KUWAIBIAJESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanamama Joyce Aluta wa Mombasa kwa kosa la kuwawekea wanaume dawa za kulevya kwenye pombe na kisha kuwaibia vitu mbalimbali kama simu, saa, viatu, wallet na pesa.

Joyce mwenyeji wa eneo la Kisimani, Nyali anadaiwa wakati mwingine kujifanya kahaba na kisha akiondoka na mteja mpaka nyumbani kwake huondoka na TV, Radio, Computer na vitu vingine.

Polisi wanamshikilia Joyce na wamefanikiwa kupata baadhi ya vitu alivyowaibia wanaume hao simu, viatu na fedha taslimu na sasa anasubiri uchunguzi ukamilike ili apandishwe kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages