KIJANA ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BIBI WA MIAKA 70


Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elias Mgaya (20) mkazi wa kijiji cha Madilu wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kosa la kumbaka bibi kizee wa miaka 70.

Akisomewa hukumu hiyo na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 32 la mwaka 2021 Elias Mgaya ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130 (1) (2)(c)na 131(1) Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

Awali akisomewa shtaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asigile imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo machi 29 mwaka huu ambapo alimvamia bibi huyo(jina lake limehifadhiwa) nyakati za usiku akiwa amelala na kisha kutenda kosa hilo.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments