JAMAA AKAMATWA AKISAFIRISHA BANGI KWA KUJIZUNGUSHIA MWILINI


POLISI katika kaunti ya Busia huko nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 40 akisafirisha misokoto ya bangi aliyoificha kwenye begi na mingine kujizungushia mwilini.

Mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Albert Wabwire amekamatwa asubuhi ya Alhamisi Desemba 30,katika eneo la Sio, akitembea kutoka Busia hadi Matayos nchini Kenya.

Polisi wanasema walipofanya upekuzi walimkuta akiwa na bangi kwenye begi alilokuwa amebeba huku kiasi kingine cha mzigo huo akiwa amefungwa kwa magunia kuuzunguka mwili wake.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Busia akisubiri kufikishwa mahakamani siku ya Ijumaa Desemba 31, 2021.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments