HALMASHAURI KUU YA CCM KUKUTANA DODOMA DESEMBA 18 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, December 14, 2021

HALMASHAURI KUU YA CCM KUKUTANA DODOMA DESEMBA 18Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu, kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kuanzia Desemba 15, 2021.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa vikao vyote ni vya kawaida kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages