ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA 'HOUSE GIRL' - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, December 24, 2021

ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA 'HOUSE GIRL'MAHAKAMA ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro imemuhukumu kwenda jela miaka 30, Elitumain John Elitumain miaka 31 mkazi wa kitongoji cha Majengo Kata ya Hedaru Wilayani Same kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 12.

Akitoa hukumu hiyo leo Desemba 24, hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Mussa Hamza amesema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo akiwa na kesi ya kumbaka binti huyo ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwake.

Hakimu Hamza amesema kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Jamuhuri wakiongozwa na waendesha mashtaka wa Serikali, Frank Masese na Samweli Flavian wamethibisha pasipo shaka kuwa kosa hilo lilitendeka Oktoba 27, 2021 huko nyumbani kwa mshtakiwa.

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria 130 (2) (e) na 131(1) vyote vikiwa ni kanuni ya adhabu mapitio ya mwaka 2019 shauri la jinai 132/2021.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages