ASKARI POLISI AUA WATU SITA BAADA YA KUGOMBANA NA MKE WAKE


Afisa mmoja wa polisi anayehudumu katika kituo cha polisi cha Kabete kaunti ya Kiambu nchini Keny amewaua watu sita kabla ya kujiua mwenyewe.

Polisi huyo kwa jina Benson Imbatu anasemekana kuhusika katika vita na mkewe kwa jina Carol kabla ya kumuua kwa kumpiga risasi.

 Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, jirani ya wawili hao alisikia mlio mkubwa wa kitu kikigongwa kisha mlio wa risasi, hali iliyofanya kukimbia katika kituo cha polisi cha Kabete kupiga ripoti.

Maafisa wa polisi walifululiza hadi eneo la tukio ndipo ikajulikana kuwa afisa huyo alikuwa amemuua mkewe kwa kumpiga risasi shingoni. 

Akiwa amejihami kwa bunduki aina ya AK47, Imbatu alianza kumimina risasi kiholela, akiwaua watu wengine watano wakiwemo wahudumu wawili wa bodaboda.

Mmoja wa wahudumu wa bodaboda akifariki akipokea matibabu katika Hospitali Kuu ya Kenyatta. Watu wengine wawili walipata majeraha na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta ambako wanaendelea kupata nafuu.

Baadaye afisa huyo alijiua kwa kujipiga risasi shingoni vilevile.

 Maafisa wa polisi walichukua bunduki iliyotumiwa kutekeleza unyama huo ambao ulithibitishwa na kamanda wa Polisi Francis Wahome.

 Katika kisa sawia na hicho, polisi mmoja katika kituo cha Ganga kule Funyula kaunti ya Busia alimuua mkewe kwa kumpiga risasi kabla ya kujiua mwenyewe kwa risasi usiku wa kuamkia Juni 24.

 Majirani walisikia mlio wa risasi majira ya saa saba usiku na walipoenda asubuhi kuangalia kichotokea, waliwakuta wawili hao wakiwa wamefariki na mwanao wa maiaka sita akiwa angali amelala kitandani.

 Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Samia Winnie Siele alithibitisha kisa hicho na miili ya wawili hao kupelekwa katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Busia.

Chanzo- Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments