BODI YA REA YATEMBELEA MRADI WA UJAZILIZI KUPELEKA UMEME KWENYE MAENEO YASIYO NA UMEME SHINYANGA

Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akiangalia Transfoma ya umeme katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini wametembelea na  kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga kwa lengo la kupeleka umeme kwenye vitongoji ambavyo havina umeme katika maeneo ambayo
 yana miundo mbinu ya umeme.

Akizungumza wakati wa Ziara hiyo leo Ijumaa Desemba 17,2021 kiongozi wa msafara wa Bodi hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela alisema lengo la ziara yao ni kutembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Ujazilizi na miradi mingine inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.

Mhandisi Songela aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa nishati ya umeme hivyo kuwaomba wananchi wanaohitaji umeme kujaza fomu na kuzipeleka TANESCO huku akiwataka watendaji wa TANESCO kufanya kazi haraka ili wananchi wapate umeme.

“Mwitikio wa wananchi kutaka umeme ni mkubwa, tujitahidi kuwaunganishia huduma ya umeme. Kasi ya kuunganisha umeme iwe kubwa ili wananchi wanufaike na nishati ya umeme”,amesema Mhandisi Songela.

Aidha ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa na kuhamasishwa kuandaa nyymba zao kupokea umeme kwa kutandaza mfumo wa nyaya kwa wale wenye uwezo na kwa wasio na uwezo wahamasishwe kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho kinapunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme majumbani.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama, Frank Mahugi ameomba TANESCO kuwapatia wananchi kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ili waweze kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary amewataka Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili wananchi wanufaike na huduma ya nishati ya umeme ili kuchochea maendeleo katika jamii.

Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika Bohari/ Stoo ya kutunzia vifaa vya mradi wa ujazilizi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.

Muonekano wa Transfoma katika Bohari/ Stoo ya kutunzia vifaa vya mradi wa ujazilizi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika chumba cha kuhifadhia Mita katika Bohari/ Stoo ya kutunzia vifaa vya mradi wa ujazilizi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika ofisi ya mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama, Frank Mahugi akiomba wananchi wapatiwe kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ili waweze kupunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme.
Afisa Mahusiano kutoka TANESCO Shinyanga Victory Emmanuel Senge akionesha namna ya kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho kinapunguza gharama za kuunganisha mfumo wa umeme majumbani.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akiangalia Transfoma ya umeme katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela na wajumbe wengine wakiwa katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.

Meneja wa Mradi wa Ujazilizi Mkoa wa Shinyanga upande wa Mkandarasi, Bryson Chengula akizungumza wakati wajumbe wa bodi ya REA wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela akizungumza katika ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakati wajumbe wa bodi hiyo wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omary akizungumza wakati wajumbe wa bodi ya REA wakitembelea Mradi wa Ujazilizi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments