SMPC YATAKA JESHI LA POLISI KUCHUKUA HATUA KWA ASKARI ALIYEFUTA PICHA ZA MWANDISHI WA HABARI DERICK MILTON




Waandishi wa habari Simiyu wazuiwa kuripoti ajali ya gari licha ya kuwepo eneo la ajali.
............................................
Nimepata taarifa toka kwa Mwandishi wa habari Derrick Milton  anayefanya kazi zake  Mkoa wa Simiyu kuwa, amezuiliwa kuripoti ajali  iliyotokea Mkoa wa Simiyu.

Derrick alifika sehemu ya tukio  mchana wa leo Disemba 26, 2021 na kukuta ajali imeshatokea, alianza kufanya coverage lakini baadaye alifuatwa na Askari  kutakiwa kuonyesha Press Card, lakini haikusaidia na alinyang'anywa simu yake aliyokuwa akiandika habari na kuchukua picha.

Ifuatayo ni taarifa iliyotoka kwa Mwandishi Derick Milton
.................................................
Majira ya Saba mchana wa leo, ilitokea ajali hapa Bariadi mjini ikihusisha gari ndogo na V8.

Nilipata tetesi kuwa gari hilo lilikuwa likimuhusisha kiongozi mkubwa wa Serikali

Nilifika eneo la tukio, nikaanza kupiga picha kwa kutumia simu yangu.

Wakati naendelea kupiga picha, Asakri mwenye sare na wengine waliovalia kirai, walinifuata na kunizuia kupiga picha.

Wakaniuliza unapiga picha wewe Nani, nikawaambia mm ni Mwandishi wa habari, wakauliza kitambulisho kipo wapi, nikatoa press card nikawapatia.

Licha ya kusoma press card yangu, waliniomba simu, nikagoma, wakalazimisha ikabidi nitoe ili kuondoa Shari, wakafuta picha zote za video mnato kisha wakanirudishia Simu.

Baada ya kunirudishia simu, walinitaka niondoke eneo la tukio na nisipige picha Tena. Kisha wakaniuliza ulipiga picha kupeleka wapi?, Nikawaambia mm ni Mwandishi wa habari.

Baada ya tukio hilo, nilianza kumtafuta RPC lakini simu yake haikuwa hewani, nikawatafuta wasaidizi wake ( Afisa Habari wa polisi mkoa) lkn hakupokea simu mpaka Sasa.

By.Derick Milton
................................................

Nafikiri kuna haja ya wadau wa habari likiwemo Jeshi la Polisi kufahamishwa nafasi ya waandishi  kwenye kufanya kazi zao  kiweledi na kutokuwa na hofu kwani waandishi wanajua namna ya kufuatilia matukio ya ajali  ikiwemo kuweka mizania kwenye habari wanazozifuatilia pamoja na kulinda bad taste ya picha zinazochukuliwa kwenye eneo la tukio bila kuathiri walaji na mhanga wa ajali na kufanya taarifa zifike kwa umma kwa lengo la kumpa taarifa mlaji.

Hii itasaidia sana kujenga mazingira rafiki baina ya waandishi wa habari na wadau wa habari.

Kushika vifaa vya mwandishi na kufuta picha habari na picha aliyozokwishaandika ni kuchukua mamlaka makubwa bila kuwa na mamlaka hayo kisheria.

Poleni waandishi wenzetu wa Simiyu

By. Edwin Soko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments