MTOTO ALIYEFARIKI MWAKA 2017 NA KUZIKWA AKUTWA AKIWA HAI...KABURI LIPO TUPU GEITA

Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji cha Ngemo kata Ngemo wilaya ya Mbogwe mkoani Geita amezua taharuki kwa kuonekana  hai tena baada ya kufariki miaka  4 iliyopita .

Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishana msaidizi  Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina  Leonard Morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama Oktoba  2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua Tarehe 12 Desemba mwaka huu. 

Katika maelezo yake, Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika kwa jina la Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku wala vipande vya kanga ambavyo mama amedai walimzikia mwanae miaka 4 iliyopita 


Sambamba na hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo kwa sasa haongei baada ya kuonekana hai huku Ulimi wake ukiwa Umekatwa.

Inaelezwa kuwa katika hali isiyo ya kawaida Mtoto  mmoja ambaye amefahamika kwa jina Leonard Morisha (11) mkazi wa Kijiji cha Ngemo, wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, aliyefariki dunia katika hospitali ya wilaya ya Geita na kuzikwa Juni 27, 2017, anadaiwa kufufuka baada ya Oktoba 2020 kuonekana wilayani Kahama na wazazi wake wamempata akiwa amekatwa mishipa ya sehemu ya ulimi na kupoteza uwezo wa kuongea.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments