ZAIDI YA WATU 50 WAFARIKI KWA KIMBUNGA MAREKANI


Gavana wa jimbo la Kentucky nchini Marekani ameonya kuwa zaidi ya watu 50 wanakisiwa kuuawa na kimbunga usiku kucha.

Andy Beshear alisema idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi 100 katika kile alichokiita kimbunga kibaya zaidi katika historia ya jimbo hilo.

Alisema idadi walioathiriwa "huenda ni kati ya 70 na 100, ni mbaya sana".

Vimbunga vinasababisha uharibifu katika majimbo kadhaa ya Marekani, huku wafanyikazi wakiwa wamekwama kwenye ghala la Amazon huko Illinois.

Zaidi ya watu 100 walikuwa ndani ya kiwanda cha mshumaa mjini Mayfield, Kentucky, wakati kimbunga kilipotua, gazeti laNew York Times liliripoti.

"Tunahofii tutapoteza makumi ya watu hao," Bw Beshear alisema.

Ghala la Amazon huko Edwardsville kusini mwa Illinois liliharibiwa wakati wa kimbunga Ijumaa usiku, mamlaka ilisema.
Huduma za dharura zimetaja kuporomoka kwa bohari la Amazon kama "tukio la majeruhi wengi"

Bado haijabainika ni watu wangapi walijeruhiwa baada ya paa hilo kuporomoka, lakini huduma za dharura za eneo hilo zimesema ni "tukio la majeruhi wengi" kwenye Facebook.

Sarah Bierman amesema mwenza wake mpaka sasa hajulikani alipo.

"Nilizungumza naye mwendo wa saa mbili usiku, muda mfupi nbaadaye nikamtumia ujumbe wa arafa, na alikuwa akielekea kwenye bohari hilo kurejesha gari la kazi. Tangu wakati huo sijampata," aliambia shirika la habari la Reuters.

"Niliamua kuja hapa ili nione kinachoendelea. Sikujua jengo liliharibiwa kiwango hiki. Nina wasiwasi sana. Nataka tu kujua kama yuko sawa," aliongeza.

Amazon inatathmini hali ilivyo na kiwango cha uharibifu, msemaji alisema katika taarifa.

Hali ya dharura imetangazwa katika jimbo la Kentucky.

Polisi wanasema kimbunga hicho kimesababish "suharibu kiasi" katika maeneo ya magharibi ya jimbo hilo. Treni iliangushwa na upepo mkali katika Kaunti ya Hopkins, Sheriff Matt Sanderso aliiambia WKYT-TV.

Chanzo-  BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments