WALIOSAMBAZA PICHA ZA UTUPU ZA RAIS MTANDAONI WAACHIWA HURU



WANANDOA wa Zimbabwe wameachiliwa huru kutoka kizuizini baada ya hakimu kufutilia mbali kesi dhidi yao kwa madai ya kusambaza picha bandia za utupu za rais wa taifa hilo katika mtandao wa WhatsApp, amesema wakili wao.

Sarudzayi Ambiri Jani, 39, na Remember Ncube, 35, walihukumiwa kifungo Juni 2020 kwa madai ya kuhujumu na kumtusi rais.

Picha hizo bandia zilionekana kumuonesha rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa akiwa utupu , huku akiwa amezibwa na kitambaa kidogo cha bendera ya Zanu-PFna barakoa ambayo ilikuwa imeficha sehemu zake za siri.

Hakimu Takudzwa Gwazemba, aliwaachilia huru wawili hao kutoka kizuizini kwasababu upande wa mashtaka ulikuwa umeshindwa kuwafungulia mashtaka mwaka mmoja baada ya kukamatwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments