Breaking

Post Top Ad

Friday, November 19, 2021

Picha : MABINTI, MAMA VIJANA 30 WAHITIMU MAFUNZO CHUO CHA VETA SFS -VTC MWAKATA, FHI 360 YAWAPATIA VIFAA KAZI VYA MIL. 42 KUANZIA MAISHA


Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga waliohitimu mafunzo ya Fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) kupitia Mradi EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR wakiandamana wakati wa Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Saluni na mapambo  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga wamehitimu mafunzo ya Fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) huku wakipatiwa vifaa vya kuanzia kazi baada ya masomo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 42 na Shirika la Family Health International (FHI 360).

Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) yamefanyika leo Ijumaa Novemba 19,2021 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga amesema Serikali ya awamu ya sita inathamini sana vyuo vya kati na kwamba kitendo cha kufundisha vijana hao kwa kuwapa ujuzi ni jambo jema kwa ustawi wa jamii kwani Masomo yanayofundishwa yanasaidia kutatua matatizo ya kila siku katika jamii.

“kupitia fani zinazofundishwa hapa vijana wanapata ajira. Fedha duniani fedha zipo nyingi, lakini wengi wanazitafuta kwa njia nyingi.. hizi fani mnazopata zitawasaidia kutatua matatizo yaliyopo katika jamii ili upate fedha”,amesema Kiswaga.

“Tunawashukuru FHI 360 na wadau wote waliofanikisha vijana hawa kufika katika chuo hiki. Na mmekabidhi vifaa vya kuanzia kufanya kazi. Baada ya kutoka hapa msiende kukaa nyumbani, fursa za kila aina ni kazi kwenu kuchangamkia fursa, Vitumieni vizuri kwa ajili ya kujipatia kipato na pindi mtakapotaka kuongeza mitaji yenu nendeni kwenye halmashauri mkaombe mikopo”,amesema Kiswaga

Aidha amewaagiza Makatibu Tawala wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuwa kipaumbele katika miradi kiwe kwa wahitimu waliosoma katika vyuo mbalimbali vya kati, hivyo vijana wapewe fursa za ajira.

“Sisi serikali tutawapa fursa, kama itawezekana vijana wasajili Kampuni ili ikitokea fursa, Mkiwa na Kampuni itawasaidia kupata tenda kubwa kubwa. Kwa kweli sisi kama serikali lazima tuwaunge mkono kwa sababu chuo hiki na vyuo vingine vya VETA kimetoa ujuzi katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii”,ameongeza Kiswaga.

“Niwapongeze sana FHI 360 na timu yenu, kazi mnayoifanya hapa mtalipwa mbinguni kwani mabinti hawa mngewaacha huko walikokuwa hali ingewa mbaya sana.. Halmashauri zote hasa za Kahama, zihakikishe zinawajua hawa wahitimu kwa majina na kufuatilia wanachokifanya katika jamii. Tunawashukuru sana wadau kwa kutusaidia kuondoa mimba na ndoa za utotoni na kuzuia maambukizi ya VVU, sisi kazi yetu ni kuhakikisha tunawaokoa watoto hawa”,amesema Kiswaga.


Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka amesema balehe na akina mama vijana hao ni sehemu ya wanufaika wa Mradi wa EPIC unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

“Tumekusanyika katika Mahafali ya 18 katika chuo hiki cha Mtakatifu Fransicso wa Asale kwa lengo la kusherehekea na kuwapongeza vijana,wasichana wanawake vijana 30 kutoka kwenye halmashauri 5 za Mkoa wa Shinyanga ambazo ni Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga, Msalala,Manispaa ya Kahama na Ushetu. Vijana hawa 30 ni wanufaika wa Mradi wa USAID EPIC chini ya FHI 360 ambao mradi unatekeleza afua za UKIMWI ngazi ya jamii”,amesema Dkt. Msuka.

Amefafanua kuwa pamoja na mambo ya UKIMWI mradi wa EPIC unahusika na masuala ya DREAMS ambayo yana lengo la kuwawezesha wasichana kwanza kwenye mabadiliko ya tabia,kujiinua kiuchumi na kufanya kazi halali za kujiingiza kipato

“Vijana hawa ambao leo tunawapongeza ni sehemu tu ya vijana ambao mradi unawahudumia, wapo vijana wengi lakini kwa namna ambavyo mradi unaweka vipaumbele na kuchambua, tumeanza na hawa vijana 30 ili wakawe mbegu na chachu ya mabadiliko na kujiamini na kujitegemea kwenye jamii zao”,amesema Dkt. Msuka

Ameeleza kuwa vijana hao walipatikana kutoka kwenye maeneo yao wanakoishi, Maafisa Maendeleo ya Jamii walishirikishwa ipasavyo,wakaweka vigezo vya kuwachagua,wakachaguliwa na wao wakaweka vipaumbele vya fani zipi wasome na wakiwa hapo chuoni wamejifunza takribani miezi mitatu na kwamba kwa namna mradi ulivyoundwa siyo mwisho wa masomo yao.

“Leo tunawakabidhi kwako kama chachu ndani ya serikali ili ukawalee,ukawatunze na ukawaendeleze kwenye fani ambazo wamesoma. Tunaamini kabisa huko kwenye halmashauri wanakotokea zipo sehemu ambazo wanaweza kupelekwa kwa ajili ya kuongeza ujuzi zaidi,wakafanya kazi zao kwa vitendo hatimaye wakanufaika na ile Kampeni ya Kitaifa ya kuwawezesha vijana kupatiwa mikopo midogo midogo na wanaweza kuanzisha viwanda”,amesema Dkt. Msuka.

Ameongeza kuwa, baada ya kuhitimu masomo ya fani hizo, vijana hawataachwa hivi hivi,watapewa vifaa vya kuanzia kufanya kazi, kila mtu aliyesoma kitu ambacho yeye alipenda kusoma atapewa vifaa aghalabu vya kuweza kufanyia kazi, vya kuweza kuanzia ujuzi wake au kuendeleza ujuzi wake.

“Kwa mfano waliosoma Computer tunawapatia Computer, Photocopy mashine na vifaa vingine vya kuanzia,wale waliosomea umeme tunawapatia vifaa vya kufanyia kazi ‘Tool box’, waliosoma masuala ya ushonaji tunawapa vyerehani,nyuzi na majola ya kwenda kuanzia kushona na vitu vingine vyote”,amesema.

Katika hatua nyingine amewataka vijana hao kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia ili kuhakikisha lengo la mradi la kupunguza maambukizi ya VVU hasa kwa vijana linafikiwa huku akiwataka kuwa msaada kwa familia zao badala ya kuwa mizigo, wakaoneshe bidii ya kufanya kazi, kuwa na tabia njema,maadili mazuri na kwamba kwa kushirikiana na wadau wanaotekeleza mradi huo wakiwemo Rafiki SDO, TADEPA, HUHESO Foundation na SHIDEPHA wataendelea kuwafuatilia mabinti hao na kadri watakavyopata fedha watapeleka mabinti wengine katika chuo hicho

Afisa Mabinti Balehe na Akina Mama Vijana kupitia mpango wa DREAMS katika mradi wa EPIC, Agnes Junga amesema mabinti balehe na mama vijana hao ni wale wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 24 walio nje ya mfumo rasmi wa shule ikiwa ni sehemu ya kuwaondoa kwenye mazingira hatarishi ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi mapya ya VVU kwa kufanya ngono.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC)Padre Thomas Njue amelishukuru Shirika la FHI 360 kwa kushirikiana na mashirika mengine katika kutekeleza mradi wa EPIC akibainisha kuwa Mradi huo umekuwa msaada kwa mabinti walio katika hatari ya kupata maaambukizi ya VVU.

“Mabinti hawa sasa ni mafundi makini, wanapokwenda watakuwa mafundi wazuri, tutaendelea kushirikiana katika kuwalea watoto hawa katika malezi bora. Vijana hawa wamekuwa wasikivu, wabunifu na walio tayari kufuata maagizo na maelekezo mbalimbali wanayopewa na walimu katika kipindi cha miezi mitatu, hakuna aliyewaza kutoroka au kuwaza kuolewa, wamemaliza masomo yao salama”,amesema.

Ametumia fura hiyo kuomba wahitimu wapewe nafasi katika miradi ya serikali, kwani vijana hao wanao ujuzi wa kutosha.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitibu wenzake, Grace Msalila amesema walichaguliwa kujiunga na masomo katika chuo hicho kupitia vikundi vya wasichana vinavyosimamiwa na Shirika la FHI 360 na kwamba mara baada ya kumaliza kozi walizosoma kwa kipindi cha miezi mitatu wataweza kujiajiri ama kuajiriwa hivyo kuondokana na hali ya utegemezi hivyo kujiepusha na vishawishi mbalimbali.

Amezitaja fani walizosoma kuwa ni Fani ya Umeme, Uchomeleaji na ufundi magari, udereva, Kompyuta, ufundi cherehani, saluni na mapambo.

“Pia tumesoma Fani za umeme, uchomeleaji na ufundi magari ambazo zilizoeleka kusomwa na wanaume pekee Hali hii inaonesha rasmi kuwa hakuna kazi inayoweza kufanywa na wanaume pekee au wanawake pekee”,ameongeza Grace.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga waliohitimu mafunzo ya Fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) kupitia Mradi EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR wakiandamana wakati wa Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama leo Ijumaa Novemba 19,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama ambapo Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga wamehitimu mafunzo ya Fani mbalimbali kupitia Mradi EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR.
akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama ambapo Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga wamehitimu mafunzo ya Fani mbalimbali kupitia Mradi EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR.
akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama ambapo Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga wamehitimu mafunzo ya Fani mbalimbali kupitia Mradi EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC)Padre Thomas Njue akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 

Afisa Mabinti Balehe na Akina Mama Vijana kupitia mpango wa DREAMS katika mradi wa EPIC, Agnes Junga akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama .
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Neema Edson akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 

Mratibu wa Mafunzo wa Chuo cha St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC Mwakata), Charles Maganga akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Grace Msalila akisoma risala kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Katiba Tawala wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama ambapo Mabinti balehe na akina mama vijana 30 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 mkoani Shinyanga wamehitimu mafunzo ya Fani mbalimbali
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Wahitimu wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Wahitimu wakiimba na kucheza kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Wahitimu wakiimba kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mwalimu wa chuo cha SFS VTC Mwakata, Magreth Alimosa akiwa amebeba Keki maalumu kwa ajili ya wahitimu katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mwalimu wa chuo cha SFS VTC Mwakata, Magreth Alimosa akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (katikati) Keki maalumu kwa ajili ya wahitimu katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Muonekano wa Keki maalumu kwa ajili ya wahitimu katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Padre Dkt. Faustine Kamugisha kutoka Bukoba akiomba wakati wa zoezi la kukata Keki maalumu kwa ajili ya wahitimu katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Wageni waalikwa wakiwa katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akikabidhi Computer kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Computer  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akizungumza wakati akikabidhi Computer kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Computer  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Uchomeleaji  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Ushonaji  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Umeme  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Ufundi Magari na Udereva katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ( wa pili kushoto) akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mabinti balehe na akina mama vijana waliosoma Fani ya Saluni na mapambo  katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama  ambapo Shirika la FHI 360 kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR limetoa vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi baada ya kumaliza masomo kwa kila mhitimu kulingana na fani aliyosomea. 
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Sehemu ya Vifaa kwa ajili ya kuanzia kazi walivyopewa Mabinti balehe na akina mama vijana baada ya kumaliza masomo katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama
Diwani wa kata ya Mwakata, Ibrahim Six akizungumza kwenye mahafali hayo
Wanafunzi wakiwa kwenye Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta (SFS VTC Mwakata Kahama.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages