Breaking

Post Top Ad

Friday, November 12, 2021

WAKAMATWA TUHUMA ZA KUMUUA BOSI WAO KISA KUTOWALIPA FEDHA ZAOWANANDOA wawili ambao walikuwa wakifanya kazi za vibarua, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumuua mwajiri wao Theopista Laurent, mwenye umri wa miaka 71 mkazi wa Kijiji cha Buharata wilaya ya Missenyi, wakidai kawatumikisha muda mrefu bila kuwalipa ujira wao.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma, amesema kuwa bibi huyo aliuawa Oktoba 15, 2021, na kwamba baada ya watuhumiwa hao ambao ni Robert Berenado (19) na mke wake Benadetha Robert (19) kumuua, walikimbia na kwenda kujificha katika Kijiji cha Kiruruma kilichoko wilayani Karagwe, na baada ya upelelezi kufanyika walikamatwa na polisi Oktoba 31 mwaka huu.

Aidha, Kamanda huyo amesema kuwa jeshi hilo linawashikilia Tawabu Ismail (35) na Joseph Laurian (42), wakazi wa Minziro wilayani Missenyi mkoani humo baada ya kukamatwa wakiwa na mfupa wa mguu na meno ya Tembo kinyume cha sheria.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages