Breaking

Post Top Ad

Friday, November 12, 2021

BINTI AUAWA BAADA YA KUGOMA KUOLEWA MAHARI YA NG'OMBE 13 KIGOMA
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu akiwemo Baba mzazi Kulwa Juakali (40) Mkazi wa Kijiji cha Lufubu wilaya ya Uvinza kwa tuhuma za kumpiga fimbo mtoto wake Mbaru Juakali ( 17) hadi kusababisha kifo chake kutokana na kile kilicholezwa kumlazimisha kuolewa kwa mahari ya ng’ombe 13 bila ridhaa yake.


“Binti alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake akilazimishwa kuolewa ambapo kulikuwa na ahadi ya kulipwa mahari ya ng’ombe 13, na waliokuwa wakishinikiza aolewe ni wazazi na hao ndiyo walikuwa na uroho wa kupokea mahari ya hao ng’ombe 13.

“Taarifa zilizopo binti huyu alikuwa anachumbiwa na wanaume watatu kwahiyo yule ambae game lilikua kubwa kwa Ng’ombe 13 huyo ndio alikua analazimishwa aolewe nae wakati binti hakuridhia na kupelelea kipigo,” amesema James Manyama RPC Kigoma.

Polisi Kigoma wanasema upelelezi wa shauri hilo unaendelea watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria akiwemo Baba mzazi Kulwa Juakali (40), Baba mkubwa wa marehemu Shija Juakali (44) na Baba mdogo wa marehemu aitwaye Majiba Juakali ( 29) wote wakazi wa kijiji cha Lufubu wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages