Breaking

Post Top Ad

Friday, November 12, 2021

HILI HAPA KABURI LA MWANAMKE 'ALIYEKUFA KWA SABABU YA FURAHA ILIYOPITA KIASI'


Kaburi jipya la Elizabeth Lingard lipo katika Great Orme, Llandudno
**

Mwanamke "aliyekufa kutokana na furaha iliyopita kiasi " mnamo mwaka 1926 amejengewa alama mpya katika kaburi lake karne moja baadaye.

Elizabeth Lingard, kutoka Llandudno, eneo la Conwy, alibaini kuwa alipata kile ambacho aliamini kuwa ni adimu katika nakala ya kwanza, na kukituma ili kiuzwe.

Bibi wa miaka 90 alianguka na kufa baada ya kumwambia mama mwenye nyumba kuwa alikuwa karibu kuwa tajiri.

Sasa kundi la watu wamekusanyika kuweka jiwe la msingi juu ya kaburi lake, ambalo lilikuwa halijawekwa alama tangu kifo chake.

Elizabeth Lingard alikuwa amesoma ripoti ya gazeti kwamba toleo la kwanza la riwaya ya Karne ya 17 The Pilgrim's Progress ya John Bunyan kilikuwa kinauzwa kwa £6,500 - zaidi ya £250,000 kwa bei ya sasa.

Na kumkumbusha kuwa alikuwa na nakala ya kitabu hicho ambacho alipewa na mama yake akiwa mtoto ,mnamo mwaka 1840.

Akiamini kuwa kitabu chake kilikuwa na thamani , aliwasiliana na mpwa wake aliyeko Warwickshire, ambaye alimwambia amtumie kitabu hicho cha thamani kuuzwa.

Alikifunga kitabu hicho na kukituma kwa njia ya posta kutoka Llandudno kabla hajarejea nyumbani, ambapo ripoti za magazeti zinasema "msisimko wake uliendelea, na kwenda kumwambia mama mwenye nyumba yake, Bibi Parry kwamba angekuwa tajiri kabla ya kufa.

"Lakini alipoanza kupanda ngazi kuelekea kitandani kwani, alianguka."

'Alikufa kutokana na furaha iliyopita kiasi'

Daktari aliitwa lakini Elizabeth Lingard alikuwa amekufa na kuzikwa katika makaburi ya Great Orme katika kaburi ambalo halikuwekwa alama yeyote.

Adrian Hughes, kutoka makumbusho ya Home Front huko Llandudno, aliandika stori katika gazeti.

"Kichwa cha habari kikiwa kimeandikwa 'amekufa kwa sababu ya furaha', ingawa Elizabeth Lingard alikuwa si mtu nilikuwa namtafuta lakini nilivutiwa kujua zaidi kuhusu yeye.

"Nilienda kutafuta kaburi lake na kukuta halikuwa na alama au kujengewa."
Bwana Hughes aliweka taarifa katika mitandao ya kijamii, na aliwasiliana na Lord-Brown and Harty, kampuni ya undertakers, ambayo ilijipanga kujengea kaburi hilo.

'Inaweza isiwe na thamani kabisa'

Jonathen Harty alisema: "Haikuwa sawa kwa mwanamke huyo kufa katika umri mkubwa akiwa ana mawazo kuwa atakuwa tajiri lakini amezikwa katika kaburi ambalo halijaweka hata alama.

"Simulizi ya mwanamke huyo , iligusa watu wengi - jiwe hilo liliwekwa bure na baraza lilitoa ruhusa kuruhusu hili lifanyike."

Adrian Hughes aliongeza: "Ni vyema kwa kundi la watu ambao hawamfahamu wameamua kumjengea kaburi vizuri miaka 95 baada ya kifo chake.

"Kitabu hicho ambacho kilibaki kwa mpwa wake Elizabeth Lingard wa Water Orton huko Warwickshire, lakini hatujui nini kilitokea baada ya hapo.

"Inawezekana hakikuwa na thamani yeyote. Tunahisi tu ,hatuwezi kujua."

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages