WATU SABA WAFARIKI , 24 HOI KWA KULA KASA ZANZIBAR - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Monday, November 29, 2021

WATU SABA WAFARIKI , 24 HOI KWA KULA KASA ZANZIBAR


Watu saba wamefariki dunia na wengine 24 wakipigania maisha yao katika hospitali moja kisiwani Pemba baada ya kula nyama ya kasa.

Kimsingi,kasa wa baharini huliwa na watu wengi katika ufukwe wa bahari lakini inasadikiwa kuwa ule ambao wakazi wa Msuka Taponi Wilaya ya Micheweni Pemba walikula ulikuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Pemba Kaskazini, Juma Sadi amepiga marufuku ulaji wa kasa baada ya kubainika kuwa nyama yake ina sumu,The Citizen imeripoti.

Alisema watatu walikufa Ijumaa , wawili walikufa Jumamosi na vifo vingine viwili vilithibitishwa Jumapili,Novemba 28.

Haikuwa wazi ikiwa wote saba walikuwa wa familia moja au vinginevyo.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi alituma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na kuwataka wawe na subra.

Social embed from twitter


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages