AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA TISHIO ZAIDI CHARIPOTIWA AFRIKA KUSINI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, November 26, 2021

AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA TISHIO ZAIDI CHARIPOTIWA AFRIKA KUSINI


Wanasayansi nchini Afrika Kusini wameingiwa na wasiwasi wa aina mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa hivi karibuni na kinachotajwa kujibadili kwa kasi kubwa na kuenea kwa haraka miongoni mwa vijana na ripoti zinasema hata chanjo haziwezi kukikabili.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ndani ya siku tano zilizopita na aina hiyo mpya ya kirusi ndiyo inahofiwa kuchochea kupanda kwa maambukizi, Wanasayansi nchini humo wanajaribu kutathimini ni asilimia ngapi ya maambukizi mapya ambayo yamesababishwa na aina mpya ya kirusi.

“Wakati timu ya wanasayansi wakifanya utafiti na kutupa taarifa zaidi mwishoni mwa juma tutakuwa na uwezo zaidi lakini bila shaka, tunaona kwamba kutokana na uzoefu wa miezi 21 iliyopita au zaidi, tunaweza kutabiri jinsi hali itakavyokuwa, kama nilivyosema, hasa wakati Delta ilivyoanza Gauteng, unaweza kuwa na uhakika kwamba watu watapoanza kutembea katika wiki chache zijazo kirusi kitakuwa kila sehemu”,wamesema

Kirusi hicho aina ya B.1.1.529, pia kimeripotiwa nchini Botswana na Hong Kong miongoni mwa wasafiri waliotoka Afrika Kusini, Wataalamu wa WHO watakutana leo kutathmini kirusi hicho na kuona kama watakipatia jina la kigiriki.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages