Breaking

Post Top Ad

Wednesday, October 20, 2021

OLE SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI TENA KESI YA UHUJUMU UCHUMI


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30, tayari leo Jumatano Oktoba 20, 2021 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha  kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi ambayo inamkabili na wenzake sita.

Sabaya amefika mahakamani saa 3:37 asubuhi leo 20, Oktoba akiwa ametulia huku akipungia mkono watu wachache ambao wamefika kusikiliza shauri lake.

Kesi ya Sabaya inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda na jamhuri inawakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Felix Kwetukia,Ofmed Mtenga na Wakili wa Serikali, Neema Mbwana.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages