Breaking

Post Top Ad

Wednesday, October 20, 2021

JAJI MUSTAPHA SIYANI AANZA KUSOMA HUKUMU NDOGO NDANI YA KESI YA MSINGI KATIKA KESI YA FREEMAN MBOWE NA WENZAKE


Jaji Mustapha Siyani ameanza kusoma uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umeanza kusomwa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 saa 4: 00 asubuhi katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Jaji Siyani amesema ataanza kusoma kwa ufupi yale yaliyozungumzwa ambayo atayaona ni ya muhimu.

Kwa ujumla Jaji Siyani kwa Sasa anafanya rejea ya ushahidi wa upande wa mashtaka kwa muhtasari.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages