MWENYEKITI WA CHAMA CHA USHIRIKA APIGWA



Watu zaidi ya 20 ambao ni jamii ya wafugaji wanadaiwa kumshambulia Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha, kwa kumpiga kichwani, mkononi kwa kutumia fimbo na vitu vyenye ncha kali na kumsababishia majeraha wakati akiwa shambani.

Tukio hilo limetokea wakati Chacha, mgambo na baadhi ya maofisa wa CHAURU wakielekea katika eneo la shamba lao lililopo Ruvu ambalo wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao mara kwa mara na kuharibu mazao yaliyolimwa.

Inaelezwa kuwa baada ya kufika shambani mgambo walipoona kundi hilo la wafugaji waliamua kukimbia kwa hofu, ndipo wafugaji hao wakapata fursa ya kumvamia Chacha na Afisa kilimo wa CHAURU Mwita Daniel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Visezi Halmashauri ya Chalinze Mohamed Musa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wafugaji kulisha mifugo kwenye shamba hilo imekuwa kawaida kwao hasa kipindi cha kiangazi.

Tayari Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu wawili jamii ya wafugaji kwa tuhuma za kumpigia na kumjeruhi Mwenyekiti wa Chama Cha Umwagiliaji Mpunga (CHAURU), Ruvu Mkoani Pwani aliyetajwa kwa jina la Sadaka Chacha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ACP Nyigesa Wankyo kuwa Oktoba 25 saa tisa alasiri katika mashamba yanayomilikiwa na Chama Cha Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) watuhumiwa hao wakiwa na wenzao watatu jumla walikua watano walilazimisha kuingiza mifugo Yao kwenye mabwawa ya kilimo cha Umwagiliaji Ili mifugo yao inywe maji.

RPC Wankyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Petro Ngilangu (25)na Robert Kambai (28) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji Cha Kidogozelo Kata ya Vigwaza.

Wafugaji hao walimshambulia Mwenyekit huyo wa CHAURU Chacha kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani.

Tukio la kupigwa lilitokana baada ya Mwenyekiti huyo akijaribu kuzuia mifugo kuingia ndani ya mashamba hayo, ambapo Sadala akiambatana na Daniel Mwita Ofisa pamoja na askari Mgambo walielekea eneo hilo.



Walipofika mashambani Askari Mgambo walipoona wamezidiwa walitimua mbio na kuwaacha wenzao ndipo wakawavamia Chacha na Mwita wakawashambulia kwa kutumia fimbo na vitu vyenye ncha kali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments