HII NDIYO FAMILIA YA WATOTO 11 WENYE MAJINA YENYE HERUFI MOJA


Picha ya familia ya Marino Vaneenoo na Gwenny Blanckaert

Familia ya Gwenny Blanckaert na Marino Vaneeno imekuwa na utamaduni wa kipekee linapokuja suala la kuwapa majina watoto wao

ambapo familia hiyo yenye jumla ya watoto 11 ( wa kike 7 na wa kiume 4) imekuwa ikitumia herufi 4 zinazofanana katika kuwapa majina watoto wao wote 11, na herufi hizo ni (A , X ,E na L).
Mtoto wa kwanza katika familia hiyo ni Alex ana miaka 13, akifuatiwa na Axel,( 12), Xela, (11), Lexa,( 10), Xael, (9), Xeal, (8),Exla, (5), Leax,( 4), Xale, (2), Elax,(1), na Alxe ambaye ana miezi 6.

Hivi karibuni wazazi hao wanatarajia kupata mtoto wao wa mwisho wa kiume mwezi Aprili mwaka 2022 ambaye atakamilisha idadi ya wototo 12.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments