Friday, October 15, 2021
MBUNGE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU
Mbunge wa chama cha conservative nchini uingereza Sir David Amess amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu katika eneo bunge lake huko Essex.
Polisi walisema mwanamume mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa kwa tuhuma za mauaji baada ya shambulio hilo katika kanisa huko Leigh-on-Sea.
Walisema walipata kisu na hawamtafuti mtu mwingine yeyote kuhusiana na tukio hilo.
Sir David, 69, alikuwa mbunge tangu 1983 na alikuwa ameoa na watoto watano.
Katibu wa Afya Sajid Javid alisema alikuwa "mtu mzuri, rafiki mkubwa, na mbunge mzuri, aliyeuawa wakati anatimiza jukumu lake la kidemokrasia".
Chanzo - BBC SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Malunde 1 blog ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.
No comments:
Post a Comment