Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Friday, October 1, 2021

HUKUMU KESI YA LENGAI OLE SABAYA NA WENZAKE KUTOLEWA LEO


Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, leo inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya jinai namba 105 ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34).

Washtakiwa wengine katika shauri hilo ni Silvester Nyegu(26) na Daniel Mbura(38), ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kesi hiyo ilinguruma kwa siku 35 mfululizo mbele ya Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Odira Amworo hadi kufikia tamati.

Upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi 11 na vielelezo 10 vya ushahidi na viliwasilishwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi.

Mashahidi wa upande wa utetezi, walikuwa watatu na walijitetea kwa njia ya kula kiapo na kuwasilisha baadhi ya nyaraka kama vilelezo vya ushahidi.Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages