Breaking

Post Top Ad

Monday, October 25, 2021

CWT YATOA MAFUNZO YA SHERIA KWA WAWAKILISHI WA SHULE NA VYUO MANISPAA YA SHINYANGA..BALELE AONYA MIKOPO UMIZA

Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Shinyanga, John Balele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya Wawakilishi 74 wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa Mafunzo ya Sheria zinazohusu Walimu ikiwemo Ajira , Utumishi, Wajibu na Haki zao.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Manispaa ya Shinyanga yamefunguliwa leo Jumatatu Oktoba 25,2021 na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga John Balele ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala amesema mafunzo hayo yamehudhuriwa na washiriki 74 wakiwemo wawakilishi wa walimu wa shule za msingi 54, shule za sekondari 14 na vyuo na taasisi nne huku akibainisha kuwa yatasaidia kupunguza changamoto mbalimbali kwenye vituo vya kazi.

Mashigala amezitaja miongoni mwa mada zitakazofundishwa katika mafunzo hayo kuwa ni Historia ya Vyama vya Walimu Tanzania, Katiba ya CWT na kanuni zake, Sera za CWT, Sheria na Kanuni zinazomhusu Mwalimu, Stadi za Uongozi, Stadi za Maisha, Fedha na mali za CWT na Mawasiliano.

Akifungua Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Shinyanga John Balele amesema mafunzo hayo ya Sheria na Stadi za Maisha yatawasaidia wawakilishi hao kwenda kusaidia kutatua changamoto na migogoro na mihemko ya baadhi ya walimu kwenye maeneo yao ya kazi ili kudumisha upendo na mshikamano.

“Sisi wenye umri mkubwa tunaondoka ndiyo maana tunaleta semina hizi ili watu wakielewe chama, waelewe misingi ya vyama vya Wafanyakazi, Wajue sheria na kanuni za mtumishi wa umma, wajue uongozi ni nini, wajue stadi za kazi ndiyo maana tupo hapa leo. Tumekuwa na hizi semina kila tunapochagua uongozi Tunaamini baada ya kutoka hapa mtakuwa mabalozi wazuri na washauri wazuri kwenye maeneo yenu ya kazi”,amesema Balele.

“Tunajua mpo nyinyi walimu wenzetu mnaotusaidia kule kwenye maeneo ya kazi kuwajenga walimu, Walimu wanapungukiwa kitu kidogo maarifa,kuna walimu tunawapoteza,baadhi ya walimu wameshindwa kuwa na maadili mazuri siyo kwamba wanapenda bali wanakosa tu maarifa ndiyo maana CWT inaendelea kutoa semina hizi kila wilaya kwa wawakilishi wa shule ili wakitoka hapa wakawasaidie walimu wengine ili kupunguza migogoro mbalimbali”,ameeleza Balele.

Balele amewataka walimu hao kwenda kushirikiana na Wakuu wa shule kubadili tabia za waalimu (kuwa shape walimu wenzao) katika sehemu zenu za kazi ili kuwa na walimu bora na walimu wazuri.

“Naamini mtaenda kuondoa mihemko ya baadhi ya walimu wetu kulingana na mazingira na kazi yetu. Vituo vyetu vya kazi ni vituo vya amani na furaha mkifanya kazi mkiwa na furaha, upendo na mshikamano”,amesema.

Aidha ameeleza kuwa mwalimu akitambua wajibu wake itasaidia kuepuka mambo yanayosababisha kuvunja mahusiano mazuri ikiwa ni pamoja na kuepuka kutowajibika, uvivu,unafiki,kugombania madaraka,kujiamini kupita kiasi na dharau.

Katika hatua nyingine Balele amewataka walimu kuepuka mikopo umiza na kuhakikisha wanajihusisha na shughuli za ujasiriamali ili kujiingizia kipato kwani Mshahara pekee hautoshi kukidhi mahitaji yao yote.

“Imefikia hatua sasa ya kukwepa watu wanaotudai na kuacha Kadi zetu za Benki kule, hili jambo limetudhalilisha sana sasa tuseme basi. Tuwaambie walimu wetu kuwa ile mikopo umiza waachane nayo mfano mtu anakopa shilingi Milioni 6 halafu anarudisha milioni 25, tumekuwa na kesi nyingi za namna hii..Tuwaambie walimu wakakope sehemu sahihi, sehemu ambazo haziumizi, kuna baadhi ya maeneo walimu wamekimbia wadeni wao, wanajificha",amesema.

“Nendeni mkawaambie walimu waangalie fursa kwenye maeneo yao wafanye, zipo fursa nyingi, upo ufugaji, kilimo na biashara zingine nyingi”,ameongeza.

Hali kadhalika amewakumbusha umuhimu wa kuendesha vyombo vya moto kwa uangalifu wakizingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni na kuvaa kofia ngumu ‘Helmet’ wanapoendesha pikipiki.

Katibu wa CWT Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe amewashauri walimu kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kuepuka kusambaza ‘kupost’ vitu visivyofaa huku akiwataka kutunza siri na kuwa na mawasiliano mazuri baina yao ili kuepusha migogoro.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Shinyanga, John Balele akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Sheria zinazohusu Walimu kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 25,2021 katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Shinyanga, John Balele akiwataka walimu kuachana na mikopo umiza wakati akifungua Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Shinyanga, John Balele akielezea faida za stadi za maisha ambazo ni:
“Kutusaidia kuwa na maadili mema, kujenga mahusiano mazuri,kuwa na maamuzi sahihi,kuwa na uwezo wa kutatua migogoro,kujengeka kwa tabia zinazofaa,kujiletea maendeleo mazuri kimasomo,kuzuia kubaguliwa katika jamii,kujenga kujiamini,kujizuia kutenda mambo mabaya ambayo ni machukizo kwa jamii”.
Mwenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala akizungumza kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala akizungumza kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CWT Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe akizungumza kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CWT Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe akizungumza kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CWT Manispaa ya Shinyanga, James Msimbang’ombe akitoa mada ya Mawasiliano kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa Chama cha Walimu Halmashauri ya Ushetu, Alphonce Mbassa akitoa mada juu ya Historia ya Vyama vya Walimu Tanzania.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Ngokolo, Daniel Togoro akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa CWT Manispaaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala akizungumza kwenye Mafunzo kwa Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Mafunzo yakiendelea ukumbini

Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wawakilishi wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo na Taasisi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages