THE CASK BAR MWANZA YATEKETEA KWA MOTO


Moto ukiteketeza bar ya The Cask

The Cask Bar iliyopo Rocky City Mall Jijini Mwanza imewaka moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 25, 2021 chanzo cha moto kikiwa bado hakijajulikana.

Mkurugenzi wa bar maarufu ya The Cask ya jijini Mwanza, Joe Makanyaga, ambayo imeteketea kwa moto  amesema kuwa ataangalia namna ya kuanza upya na wafanyakazi ambao alikuwa anafanya nao kazi tangu mwanzo.

Joe amesema kuwa moto huo umegharimu kwa kiasi kikubwa maisha ya wafanyakazi pamoja na yeye kibiashara na kusema kwamba yeye kama mfanyabiashara anatambua uwepo wa hasara za namna hiyo na kwamba huo siyo mwisho wa bar hiyo bali ataanza upya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments