BILIONI 15.9 KUGHARIMU TAFITI YA UVIKO-19

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi 

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog Dodoma

WIZARA ya Afya imeanza kujikita  kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Corona na kuwajengea uwezo watalaam wa afya utafiti utakaogharimu Shilingi bilioni 15.9 ikiwa ni pamoja na  kufanya tafiti sita (6) kuhusu tabia za virusi za virusi vya Corona kwa kuangalia askari wa kinga mwili (antibodies), uelewa, mtazamo na utendaji,utafiti wa kimatibabu, kuchunguza mpangilio wa vinasaba,hali ya kimelea kubadili hali/vinasaba vyake vya awali na utafiti wa tiba asili.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dodoma na  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi wakati akiongea na Waandishi wa habari na kufafanua kuwa kati ya Shilingi, bilioni 466.781, Shilingi  bilioni 259.228 zitasimamiwa na Wizara hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi iliyoko chini yake pamoja na Taasisi na Hospitali huku Shilingi 207.643 zitasimamiwa na OR - TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji miradi ya afya iliyoko chini ya OR - TAMISEMI ikijumuisha vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi ya Msingi (Halmashauri) kuanzia hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati.

Amesema ili kufanikisha tafiti hizo inajenga na kukarabati Hospitali sita za Rufaa za Mikoa ya Lindi, Songea, Kigoma, Mtwara (Ligula), Tabora (Kitete), Katavi, Ukerewe na Taasisi ya afya ya akili Mirembe na kwamba matokeo ya tafiti hizo yatawezesha Serikali kufahamu aina ya kirusi kilichopo nchini ili kufanya vipimo na kutoa chanjo.

Amefafanua kuwa hatua hiyo pia itasaidia  kufahamu sababu za muitikio mdogo  wa jamii katika kupata chanjo ya UVIKO - 19 hivyo kuishauri Serikali njia sahihi ya kuongeza muitikio; kufahamu ufanisi wa dawa za asili katika kupambana na UVIKO - 19 na kuishauri Serikali; Kufahamu madhara ya UVIKO - 19 kwa wagonjwa wanaopata maambuki; kufahamu  viambata vilivyopo kwenye dawa za asili ambavyo vinasababisha utibabu wa korona na kufanya ugunduzi wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 .

Amesema uwekezaji huo unategemewa kuwa na faida kwa  kupunguza vifo vya wagonjwa kwa asilimia 20-40% ndani ya vituo vya afya, kuimarisha huduma za maabara, mionzi na tiba mtandao; itakayogharimu Shilingi bilioni 111.5 ambayo itasaidia ugunduzi wa haraka wa magonjwa mbalimbali,kupunguza rufaa kwenda Hospitali ya Taifa na kuimarisha huduma za chanjo dhidi ya UVIKO - 19 , elimu ya afya kwa umma dhidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo itakayogharimu Shilingi bilioni 43.2. hivyo kuwezesha kuwakinga Wananchi wengi dhidi ya vifo vinavyohususiana na UVIKO-19.

"Kupitia fedha hizi tunaimarisha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za Afya itakayogharimu Shilingi bilioni 41.8 na hivyo kupanua na kuboresha huduma za kibingwa katika ngazi ya mikoa na Kanda lakini pia kufanya tafiti za kitaalam kuhusu Virusi vya Korona pamoja na kuwajenga uwezo watoa huduma za Afya itakayogharimu Shilingi bilioni 15.9. 2.1,"amesema.

Prof. Makubi pia ametumia nafasi hiyo kueleza namna malengo hayo yanavyotekelezwa ambapo alisema  Sekta hiyo imeaza michakato ya  kukarabati na kujenga majengo ya matibabu ya dharura (EMD) 102, vitengo vya wagonjwa wanaohitaji uangallizi maalum (ICU) 67 na kusimika vifaa vyake.  

Aidha amesema ,Hospitali ya Taifa itakarabati ICU 2, Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (ICU 5 na EMD 1); Hospitali za Kanda (ICU 5 na EMD 4); na katika ngazi ya mikoa na Halmashauri (ICU 30 na EMD 80) chini ya OR TAMISEMI.

"Fedha hizi poa zitaimarisha mfumo wa rufaa kwa kununua na kusambaza magari 253 ya kubebea wagonjwa, kati ya magari hayo magari 20 ‘advanced ambulances’ yatapelekwa katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (1), KIA (1), Mwanza Airport (1), Hospitali ya Mzena (1), Hospitali za Rufaa za Mkoa (8), Hospitali za Kanda (6), Hospitali Maalum na Ubingwa Bobezi (5);

Magari 233 ni ya kawaida (basic ambulances) na yatapelekwa Hospitali za Rufaa za Mkoa (38) na magari 185 katika ngazi ya OR TAMISEMIKuimarisha upatikanaji wa damu salama kwa kununua na kusambaza 8 ya kisasa (mobile blood collection vans) kwenye kanda Kanda ya Ziwa - Mwanza; Kanda ya Mashariki - Dar es Salaam; Kanda ya Nyanda za Juu Kusini-Mbeya; Kanda ya Kusini - Mtwara; Kanda ya kaskazini - Kilimanjaro; Kanda ya Magharibi - Tabora; Kanda ya Kati - Dodoma; Kanda Maalum ya Jeshi na ofisi za Makao Makuu Dar Es Salaam,"amefafanua.

Pamoja na mambo mengine Katibu huyo amesema kupitia uboreshaji huo hali ya  upatikanaji wa hewa tiba ya oksijeni itaimarika  kwa kununua mitambo 10 ya kuzalisha hewa hiyo na kuisimika kwenye vituo vya kimkakati vya kutolea huduma za afya zikiwemo vituo vilivyo mbali na hospitali za mikoa iliyosimikwa mitambo tayari na vile vyenye idadi kubwa wagonjwa na kwamba mitambo minne (4) itasimamiwa na Wizara ya Afya wakati mitambo 6 itasimamiwa na OR TAMISEMI.

"Ili kufanikisha yote haya,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa wito kwa Taasisi na vituo vyote vya kutolea huduma za afya zitakazotekeleza miradi ya sekta kuzingatia, Sheria, Kanuni, taratibu na maelekezo ya viongozi katika kutekeleza miradi hiyo,hali hii itawezesha hata huduma za upasuaji kwa kununua na kusambaza mashine 60 za kutolea dawa za usingizi na ganzi pamoja na vifaa vingine muhimy vya vyumba vya upasuaji (theatre) katika vituo vya kutolea huduma za afya.  2.1.2,kuimarisha huduma za uchunguzi wa kimaabara, mionzi na tiba mtandao; Shilingi bilioni 111.5,"amesema.

Katika huyo pia Prof.Makubi ameeleza kuwa sekta hiyo inafanya mambo kadhaa kuimarisha uwezo wa ya Maabara ya Taifa na Maabara nyingine nchini ili kupima na kutoa majibu ya sampuli kwa wakati na kununua  vitendanishi vya kupima sampuli katika maabara za mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Mara, Dodoma, Arusha (Mt. Meru), Tanga na Mtwara.  

Aidha ili kuwezesha utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli kwa wakati, amesema sekta hiyo  itaimarisha Mifumo ya Ki-elektroniki ya kutolea taarifa katika Maabara Kuu ya Taifa na kuimarisha huduma za uchunguzi wa mionzi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hizo wakiwemo magonjwa wa kansa, moyo, kifua kikuu na mifupa. 

Amefafanua kuwa Sekta hiyo pia  itanunua na kusimika mashine 95 za X – Ray za kidigitali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (2), Hospitali ya Kanda Chato (1) na Mtwara (2), Hospitali za Rufaa za Mikoa 20 na X – Ray 70 zitasimamiwa na OR TAMISEMI,sekta itanunua na kusimika CT – Scan 29 ambapo;  Hospitali ya Taifa Muhimbili (1), Hospitali za Kanda ya Chato (1) na Mtwara (1), Hospitali ya Jeshi Lugalo (1), hospitali ya Uhuru (1) na Hospitali 24 za Rufaa za Mikoa na Mashine 4 za MRI zitanunuliwa na kusimikwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (1), za Kanda ya Mtwara (1), Hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean (1) na Hospitali ya Kanda Chato (1).

 "Serikali itanunua mashine 7 za huduma za uchunguzi wa moyo (Portable Echo Cardiography) kwa ajili ya Hospitali za Kanda 6 pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), sekta inaimarisha huduma za tiba mtandao (Telemedicine) kwa kukarabati na kuweka vifaa katika vitovu maalum vya Huduma ya Tiba Mtandao (Telelmedicine Hubs) kwenye Taasisi nne za Rufaa za Ubingwa Bobezi ambazo ni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, na Taasisi za Kanda ya Ziwa Bugando na Benjamin Mkapa Dodoma,"amesema Katibu Mkuu huyo.

Vilevile ameeleza kuwa katika hospitali zote za Rufaa za Mikoa kutafanyika ukarabati wa vyumba maalum vya Huduma ya Tiba Mtandao (Regional Telelmedicine centre Rooms) ambavyo vitaunganishwa kwa njia ya Mtandao na Vitovu (Hubs) zilizoko kwenye Hospitali za Rufaa za Kanda na zile zilizoko kwenye Hospitali Maalumu za Ubingwa Bobezi.  2.1.3.,kuimarisha na kuhamasisha jamii kupata chanjo dhidi ya UVIKO - 19 pamoja na kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

"Shilingi bilioni 43.2 Sekta ya Afya inaimarisha upatikanaji wa huduma za chanjo ya UVIKO Р19 kwa:-Kugomboa, kutunza na kusambaza takribani dozi milioni 1.16 kutoka Mpango wa COVAX Facility Initiative. Vilevile sekta itanunua chanjo dozi 311,765 iwapo zitahitajika tofauti na zile zinazotolewa na COVAX Facility,"amesema ̱a kuongeza;

Tutaendele kuhamasisha jamii kujikinga na maambukizi ya UVIKO - 19 na magonjwa mengine ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza,tutaboresha miundombinu katika vituo vya kutolea huduma za Afya; Shilingi bilioni 41.8,Sekta yetu pia inaboresha mazingira ya utendaji kazi na vituo vya kutolea huduma ambapo,"amesema.

Prof. Makubi pia amebainisha kuwa Serikali inajenga nyumba 176 za watumishi zenye uwezo wa kuchukua familia tatu, ambapo nyumba 26 zitajengwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na ujenzi wa nyumba 150 utasimamiwa na OR TAMISEMI.

MIKAKATI INAYOTUMIKA KUTEKELEZA MALENGO YA MIRADI 

Ili kutekeleza miradi iliyopangwa kwa muda mfupi uliopo wa kuanzia Oktoba, 2021 mpaka Juni 2021 Katibu Mkuu Prof. Makubi amesema sekta ya Afya nchini itatumia mikakati, mbinu na njia mbalimbali ambazo zimejikita katika; Uratibu, uendeshaji na usimamizi wa miradi; Taratibu za manunuzi na Ugavi; Mtiririko wa fedha (flow of funds), na Ufuatiliaji na tathmini ya miradi. 

Amesema maeneo hayo ya kimkakati hayatawezesha sekta kukamilisha malengo ya miradi kwa wakati bali miradi yenye ubora, viwango stahiki na yenye kuzingatia thamani ya fedha za Serikali,Uratibu, Uendeshaji na Usimamizi wa miradi,timu za Uratibu na Kazi, Uendeshaji na Usimamizi wa miradi zimeundwa katika ngazi ya Makao Makuu (WAMJW ; Hospitali ya Taifa Muhiimbili, Hospitali Maalum, bingwa na bobezi, Hospitali za Kanda na Hospitali za Rufaa za Mikoa  .

Akizungumzia taratibu za manunuzi na ugavi amesema yanajumuisha manunuzi ya ujenzi, vifaa na vifaa pamoja na huduma mbalimbali za miradi,  maelekezo ya Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma kupitia barua yenye Kumb. Namba CA.192/211/01/74 ya tarehe 12/10/2021, Sheria, Kanuni na miongozo ya manunuzi zitafuatwa ili kupata thamani ya fedha, ubora na viwango stahiki kwa miradi itakayotekelezwa chini ya sekta ya afya.

Amesema hali hiyo itasaidia kupunguza urasimu na pia kuweka uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. 3.4.Ufuatiliaji na Tathmini Sekta imejipanga katika usimamizi, ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali na kupima utendaji wa watekelezaji wa miradi, hatua za utekelezaji na changamoto zinazoikabili miradi ili kuzitatua kwa wakati na kuepuka kusimama kwa miradi katika sekta. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments