Breaking

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

MKE AMTUKANA KISHA KUMCHOMA KISU MME WAKE UGOMVI WA MAPENZI SHINYANGA


Mfano wa kitu chenye ncha kali
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga mwanamke aitwaye Amina Hamis (32) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumchoma kitu chenye ncha kali kichwani na tumboni mme wake aitwaye Simon Robert (43) kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Oktoba 18,2021 majira ya saba katika kitongoji cha Katunda kijiji cha Bugayambelele Kata ya Kizumbi ndani ya manispaa ya Shinyanga.

“Simon Robert (43) mkazi wa Katunda alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani na tumboni na mke wake aitwaye Amina Hamisi (32) mkazi wa Katunda na kusababishiwa majeraha”,amesema Kamanda Kyando.

“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi ambapo mbinu iliyotumika ni kumpa maneno makali kisha kumchoma na kisu”,amesema Kamanda Kyando.

Amesema mtuhumiwa amekamatwa na majeruhi amelazwa hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya.

“Napenda kutoa rai kwa wananchi wote kujiepusha na huu wivu usiokuwa na maana yoyote mbele ya sheria. Huyu mtuhumiwa ni mhalifu kama wahalifu wengine lazima sheria ichukue mkondo wake”,amesema.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages