Breaking

Post Top Ad

Tuesday, October 26, 2021

AJINYONGA KWA SHUKA AKIACHA UJUMBE 'MAISHA MAGUMU YAMENIFANYA NIJIUE,MNIZIKE'


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao

Kijana Michael Paul (18) mkazi wa Luanzari, Kata ya Ng'ambo, Manispaa ya Tabora, amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga na shuka chumbani kwake na kuacha ujumbe akimuomba msamaha mama yake na kusema maisha ndiyo chanzo cha yeye kujiua hivyo amzike.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 24, 2021, na taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo zilitolewa na dada wa marehemu aitwaye Jane Paul.

Kamanda Abwao amesema marehemu kabla ya kujinyonga aliacha ujumbe wa maandishi uliosomeka "Mama naomba unisamehe ni maisha tu yamenifanya nijiue mnizike''.

Chanzo cha tukio kimetajwa kuwa ni msongo wa mawazo, na mbinu aliyotumia ni kujifungia chumbani kisha kujitundika juu ya kenchi kwa kutumia shuka.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages