RAIS SAMIA AWAPA VIWANJA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TANZANIA


Rais Samia (katikati) akiwa na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars na viongozi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewapatia viwanja jijini Dodoma wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars kwa kuibuka mabingwa wa COSAFA 2021.

Rais Samia ametoa zawadi hiyo leo Oktoba 27, 2021 alipowaalika kwaajili ya kupokea kombe hilo pamoja na kupata chakula cha mchana.

''Nitawapatia watoto wangu wa Twiga Stars Viwanja vya kujenga nyumba zao, vitakuwa kule Dodoma ambako na mimi mama yenu naishi,'' amesema Rais Samia Saluhu.

Aidha amesisitiza kuwa soka la wanawake linatakiwa kupewa kipaumbele kama ilivyo kwa upande wa wanaume.

''Soka la wanawake limeanza miaka ya hivi karibuni lakini mafanikio yenu yameanza kuwatetemesha wanaume. Mimi huwa nasema timu ya wanawake imefanya vizuri mara kadhaa lakini hakuna anayesimama kuwasifu, lakini wanaume wakishinda tu nusu fainali sifa zinapasua anga,''.
Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia ubingwa wa COSAFA Oktoba 9, 2021 nchini Afrika Kusini

Twiga Stars walitwaa ubingwa kwenye michuano hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini, ambapo katika fainali iliyopigwa Oktoba 9, 2021 dhidi ya Malawi walishinda goli 1-0.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments