Breaking

Post Top Ad

Wednesday, October 27, 2021

JAMAA ALIYEFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MBUZI ASEMA ALIZIDIWA TU NA HAMU

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera kamishna msaidizi wa polisi Jumaa Awadhi, kulia ni  picha mnyama mbuzi (siyo wa kwenye habari)

Na Ashura Jumapili,Kagera.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera  linamshikilia Emmanuel Zakaria (38) Mkazi wa Lusahunga Wilayani Biharamulo Mkoani humo kwa kosa la kufanya mapenzi na mbuzi jike mali ya Jacobo Nyawenda (37).

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera kamishna msaidizi wa polisi Jumaa Awadhi amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24,2021 majira ya saa tisa alasiri katika kijiji cha Lusahunga kata na tarafa ya Lusajunga wilayani Biharamulo ambapo mtuhumiwa Emmanuel Zakaria ,alimchukua Mbuzi huyo aliyekuwa amefungwa malishoni kisha kumpeleka vichakani na kuanza kufanya naye mapenzi .

Amesema wakati akiendelea na kitendo hicho ,ndipo alipita mke wa jirani yake na mlalamikaji na kumkuta mtuhumiwa anafanya mapenzi na mbuzi akatoa taarifa kwa wananchi wengine na mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi hao.

Kamanda Awadhi amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi alikiri kufanya tukio hilo na kudai kuwa alizidiwa na tamaa za mwili. .
Amesema  chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na kwamba mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kituo cha polisi Biharamulo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages