Breaking

Post Top Ad

Friday, October 22, 2021

AMUUA MWENZAKE WAKIBISHANA NANI ALIPE NAULI YA BODABODA
KWELI dunia ina mambo…. Jeshi la Polisi nchini Kenya, Jeshi la Polisi ncini Kenya wanamshikilia mshukiwa wa mauaji ambaye aanadaiwa kumdunga swahiba wake kisu shingoni na kumuua papo hapo, baada ya kutofautiana.

Mshukiwa huyo Daniel Waithera, 25, alimuua rafiki yake Michael Mukami, 21, kufuatia mvutano kuhusu ni nani anayetakiwa kulipa nauli baada ya kubebwa na pikipiki.

Kulingana na mwendeshaji wa bobaboda nhini humo, Stephen Mwango, aliwabeba wawili hao majira ya saa 11:30 asubuhi kutoka Soko la Gikambura, Kikuyu katika Kaunti ya Kiambu.

Hata hivyo, walipofika Muthangari, abiria hao wawili walianza kuvutana kuhusu ni nani aliyestahili kulipa nauli. Kisha mshukiwa aliingia nyumbani kwake na kurejea na kisu chenye ncha kali.

Punde si punde, alimdunga kisu marehemu kwenye upande wa kushoto wa shingo lake na kisha kutoroka akimuwacha maiti.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages