WAZIRI BASHUNGWA NDANI YA VIWANJA VYA USHIROMBO SEKONDARI MKOANI GEITA KUHITIMISHA DOTO CUP 2021 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Saturday, September 4, 2021

WAZIRI BASHUNGWA NDANI YA VIWANJA VYA USHIROMBO SEKONDARI MKOANI GEITA KUHITIMISHA DOTO CUP 2021


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akisaliamiana na wachezaji kabla ya mechi ya fainali baina ya timu ya Namonge FC na Ituga FC zote za wilaya ya Bukombe  ambazo zinachuana kumtafuta mshindi katika mashindano ya Doto Cup 2021.

Mshindi katika mashindano hayo yanayofanyika wilaya ya Bukombe katika jimbo la Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ambaye ndiye mdhamini mkuu wa mashindano hayo, mshindi ataibuka na kitita cha shilingi milioni moja, mipira na jezi pea tatu pamoja na medali.

Mashindano ya Doto Cup yanayolenga kukuza vipaji na kuwakutanisha vijana kwa kujenga umoja na mshikamno yalizunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na yanaaminika kuwa mashindano makubwa ya mchezo wa soka kwa mkoa wa Geita.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages