WATU WENYE ULEMAVU WAMPONGEZA DC JASINTA MBONEKO KUJALI MAKUNDI MAALUMU - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Saturday, September 4, 2021

WATU WENYE ULEMAVU WAMPONGEZA DC JASINTA MBONEKO KUJALI MAKUNDI MAALUMU


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na kikundi cha Ujasiriamali cha watu wenye ulemavu kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu, Shinyanga

SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA), limempongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa kujali makundi maalum na kuwatatulia changamoto ambazo zinawakabili.

Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Richard Mpongo, ametoa pongezi hizo jana wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Shinyanga, alipotembelea kikundi cha Ujasiriamali cha watu wenye ulemavu kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga, kusikiliza changamoto zao, pamoja na kuwapatia elimu ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO -19.

Mpongo ambaye pia ni katibu wa kikundi hicho, alisema kiongozi huyo ni mfano mzuri wa kuigwa, sababu ya kujali makundi maalum kwa kusikiliza matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi, ikiwamo na kujali afya zao, ambapo ameambatana na wataalam wa afya na kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi vya virusi vya Corona, elimu ambayo hawajawahi kuipata.

“Tunamshukuru sana Mkuu wetu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa kujali watu wenye ulemavu, ambapo tumekuwa tukipata mikopo ya Halmashauri asilimia 2 bila ya kikwazo chochote, na sasa tunafanya shughuli za ujasiriamali na kutuingizia kipato,”amesema Mpongo.

“Leo amekuja na wataalam wa afya kutupatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, elimu ambayo hatujawahi kuipata, na sasa tupo tayari kupata chanjo ya UVIKO 19,”ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha ujasiriamali cha watu wenye ulemavu Suzan Masunga, ambao wanajishughulisha na Ufugaji wa Nguruwe, alisema changamoto kubwa ambayo inawakabili kwa sasa ni ufinyu wa eneo la kufuga mifugo hiyo, na kumuomba Mkuu huyo wa wilaya awatafutie eneo kubwa, ambalo pia ni rafiki kwao kufika kwa urahisi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alimwagiza Mkuu wa idara ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga John Tesha, kuwatafutia eneo la kufuga mifugo yao, pamoja na kutenga kiasi kingi cha fedha kwenye bajeti yao, ili kuwapatia mikopo watu hao wenye ulemavu asilimia 2 na kufanya shughuli za kuwaingiza kipato.

Katika hatua nyingine, alisema ameshamwagiza Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga, kutoa elimu ya Corona kwa watu wenye ulemavu, pamoja na kuwafuata mahali walipo na kuwapatia chanjo ya Corona UVIKO 19.

Pia alitoa wito kwa wadau kuwasaidia vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona watu hao wenye ulemavu, zikiwamo Barakoa, na Vitakasa Mikono (Sanitize), ili kutembea nazo mifukoni, na pale wanapokuwa wakiomba msaada na kulazimika kushindwa mikono wawe wanapaka na kuwa salama zaidi.

Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Shinyanga (SHIVYAWATA), Richard Mpongo, ambaye pia ni Katibu wa kikundi cha Mshikamano cha Ujasiriamali kilichopo Kitangili, akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwa kujali Makundi Maalum na kuwatatulia changamoto zao.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Suzana Masunga, naye akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa kuwajali, kutatua changamoto zao Pamoja na kuwapatia Elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona UVIKO-19.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na kikundi cha Ujasiriamali cha watu wenye ulemavu kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Afya wa Kata yaKitangili Manispaa ya Shinyanga Everia Raphael, akitoa elimu ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa watu wenye ulemavu.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa Sare ya Vitenge kwa ajili ya kukindi hicho kiwe kina vaa sare hizo hasa pale wanapotembelewa na wageni, akipokea sare hiyo ni Mwenyekiti wa Kikundi Suzana Masunga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimpatia Sare ya Kitenge Mwenyekiti wa SHIVYAWATA mkoani Shinyanga Richard Mpongo, ambaye pia ni Katibu wa kikundi hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendelea na zoezi la kugawa Sare za Vitenge, kwa wanakikundi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko) wa nne kutoka kulia), akipiga picha ya pamoja na kikundi cha ujasiriamali cha watu wenye ulemavu, akiwa na maafisa kutoka Serikalini.

Na Marco Maduhu-Shinyanga.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages